Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali ipo katika mchakato wa Mageuzi ya Sera ya Elimu itakayoruhusu mkondo wa Mafunzo ya Amali katika skuli za sekondari ili kuweza kuwandaa vijana mapema katika Nafasi za kujiajiri wenyewe.
Ameyasema hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt Bakari Ali Silima wakati wa Hafla ya Kuwapongeza washindi wa Shindano la Uandishi wa Insha NA washindi wa Michezo ya Elimu bila Malipo kwa Mwaka 2024 kupitia Vyuo vya Amali, huko Mkoa wa Kusini Unguja Katika Chuo cha Mafunzo ya Amali Makunduchi.
Amesema Madhumuni makubwa ya kujengwa kwa vyuo vya Amali ni kuwasaidia vijana kupata Taaluma na ujuzi ambao utawasaidia kujiajiri wenyewe.
Dkt Bakari Alisisitiza kuwa Mageuzi ya Elimu yatanzia Sekondari ili vijana waanze kupata ujuzi wa Mafunzo ya Amali mapema ili kuweza kuwa mahiri na mwishoni kuweza kujiajiri. Aidha SERIKALI ya Mapinduzi kupitia Wizara ya Elimu inampango wa kujenga vyuo vipya katika kila wilaya ili kuboresha Mafunzo haya ya Amali.
Pia Mkurugenzi Huyo amewataka vijana hao kujifunza ujuzi zaidi ya mmoja jambo ambalo litawasaidia kupata Ajira hizo kirahisi kupitia sehemu mbalimbali ikiwemo sehemu za Mahotelini
Kupitia hafla hiyo iliowajumuisha washindi wa shindano la Uandishi wa insha, jumla ya washindi watatu (3) walikabidhiwa zawadi hizo ikiwemo fedha Taslimu, vyeti vya Ushindi nk. Na kwa Upande Washiriki wa Michezo ya Elimu bila Malipo jumla ya vyuo na vituo kumi na nne (14) ikiwemo Mafunzo Vtc, ZOI Vtc, Microtech vtc, Almubarak Vtc, Mwanakwerekwe Vtc, Green Women Vtc no vilikabidhiwa vyeti vya ushiriki