Vitongoji Pemba -28 Julia 2025
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Rashid Hadidi Rashidi Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuweka vipaumbele kujenga na kuimarisha vituo vya Mafunzo ya Amali ili kutoa fursa kwa vijana kupata Mafunzo ya Amali na kuweza kujitegemea .
Akizungumza katika Sherehe za Mahafali ya kumi na moja (11) ya wahitimu wa chuo cha Mafunzo ya Amali pamoja na kuwakabidhi vyeti huko Vitongoji,
Mhe. Rashid Amesema Serikali imekuwa ikiwezesha chakula cha dakhalia, karakana na vifaa vya kujifunzia kivitendo ili vijana waweze kuishi vyuoni na kujifunza fani mbalimbali kwa lengo la kujiajiri na kujikomboa katika maisha yao ya baadae .
Mapema Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt Bakari Ali Silima, Amewataka wahitimu hao kuzitumia fursa za mikopo ili kupata mtaji wa kujiendeleza miradi yao .
Katika Risala ya wahitimu hao iliyosomwa na mwanafunzi khamis suleiman Nasour, Amesema Elimu ya Mafunzo ya Amali ni muhimu sana kwani inatengeneza msingi mzuri wa kujiajairi.
kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji Ndugu Biubwa Mohd Mselem Amesema chuo kimepata mafanikio makubwa tokea kuanzishwa kwake huku Mratibu wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Pemba Othman zaidi othman akisema mkakati madhubuti unahitajika ili kuongeza vyuo vyengine kutokana na mwamko wa vijana kujiunga na vyuo hivyo.
Mapema Mhe Rashid ametembelea mabanda ya maonyesho ya kazi za vitendo zilizoandaliwa na wanafunzi hao pamoja na kupokea maandamamno ya wahitimu.
Jumla ya wahitimu 108 wametunukiwa vyeti vya Mafunzo ya Amali kwa fani za Uhunzi, Ushoni, Uchoraji na Mapambo, Upishi, Umeme wa Majumban na viwandani nk.