The Revolutionary Government of Zanzibar
VOCATIONAL TRAINING AUTHORITY

Mahafali ya Kumi na Moja(11) Chuo cha Mafunzo ya Amali Mwanakwerekwe.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uchumi na Uwekezaji Rashid Ali Salim Amesema Serikali itaendeleza miradi iliyoibuliwa na wanafuzi wa Mafunzo wa Amali kwani inaleta tija maslahi ya taifa na ndio chachu ya Maendeleo.

Ameyasema hayo wakati akiwatunuku vyeti wanafunzi waliohitimu Mafunzo ya Amali katika fani mbali mbali katika Mahafali ya kumi na moja (11) ya Chuo cha Mafunzo ya Amali Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi A Mkoa wa Mjini Maghribi.

Alisema Umuhimu wa kupata Elimu ya Ufundi ni mpana sana kwa maslahi ya Taifa, kijamii na hata kwa mtu mmoja mmoja.
Kwani Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hupata fahari ya kujitosheleza kuwa na wataalamu na mafundi wake wa ndani katika kukuza kiwango cha uzalishaji wa ndani na hupelekea kupatikana miradi mikubwaa ya kuleta maendeleo ya Taifa.

Aliwataka wahitimu hao kufanya kazi kwa bidii na kujituma na kuachana na kufanya kazi kimazoea jambo ambalo linarejesha nyuma kimaendeleo na kuondokana na changamoto ya utegemezi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Mafunzo Amali Zanzibar Dkt Bakari Ali Silima alisema kuendesha mafunzo ya Amali ni gharama na yanahitaji mafunzo mengi ya vitendo kwa asilimia 70 hivyo wizara inajitahidi kusimamia mafunzo hayo na kufikiwa lengo la Serikali la kuwawezesha, inaandaa vijana waweze kujiajiri na kuajirika.

Aliomba Serikali kuwatumia wabunifu hao sambamba na kuwashika mkono katika yale yote ambayo wanafunzi wameyabuni ili ziweze kuleta manufaa kwa nchi yetu.

Alitumia fursa hii kuwataka wazazi wawelete vijana katika vyuo hivo kwani Mamalaka ina lengo la kutoa mafunzo hayo kwa mwaka 2026 kwa vijana elfu tatu na miatano 3,500 kwa lengo la kuwaendeleza vijana waweze kujitegemea kichumi.

Aliongeza kuwa Mamlaka ina mpango wa kwenda kuwaandikisha vijana wao katika mfuko wa bima ya afya ili kutatua changamaoto ya kiafya.

Akitaja changamoto za chuo Mwalimu Nuru Mobammed Uwesu alisema kutokana na wimbi kubwa la wanafunzi wanalazimiaka kuwaacha zaidi wanàfunzi 100 kutokana na ufinyu wa nafasi uliopo chuoni hapo.

Aidha uchakavu wa miundombinu wa majengo pamoja na uhaba wa viti, hivo wamomba Serikali kuwatatulia changamoto hii ili kuweza kuendesha shughuli zao za kielimu kwa ufanisi zaidi.

Akisoma risala ya wahitimu hao Mwanafunzi Aliy Suleiman Rashid, Amesema Mafunzo ya Amali ni muhimu kwani yamewafanya kuwa weledi na wabunifu ili waweze kujiekeza na kuondokana na utegegemezi wa kiuchumi
“wakati tunaaza tulikua hatujui kitu lakini baada kukamilika mafunzo tumekuwa weledi na wabunifu na tuko tayari kukabiliana na soko la ajira “
Alisema Mbali na mafunzo hayo pia wamepata ujuzi kuweza kuendana na mabadiliko ya soko la ajira sambasmba na kuzingatia suala la dini katika kuhakiksha wankua na maadili katika kazi zao.

Walisema kuwa mafunzo hayo hayakuwa ni ya darasani tu bali yalikua ya vitendo zaidi jambo ambalo lilowafanya kuwa bora zaidi.

Wahitimu hao waliomba Serikali Kuanzishwa kwa Diploma ya ushoni kwani kwa sasa hakuna chuo hicho jambo linalowarejesha nyuma kielemu.

Akitaja changamoto kuwa ni kukosekana kwa huduma za afya hivyo wametaka Serikali kuwaingiza katika mfumo wa bima wa serikali ili na wao waweze kukabiliana na changamoto wanazokumbana nazo wakiwa mafunzoni.

Chuo cha Mafunzo ya Amali cha Mwanakwerekwe, kinatoa Mafunzo ya Amali ya fani 5 za; Elektroniki, Ushoni, Umeme, TEHAMA na Useremala ambapo jumla ya wanafunzi 145 wamehitimu mafunzo hayo na kukabidhiwa vyeti.

Scroll to Top