The Revolutionary Government of Zanzibar
VOCATIONAL TRAINING AUTHORITY

Mahafali ya Tatu (3) Chuo cha Mafunzo ya Amali Daya.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, imeweka kipaumbele katika kuwapatia vijana wake Elimu na Stadi za kazi zitakazowajengea misingi imara na bora ya maisha yao kupitia Mafunzo ya Ameyasema hayo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhammed Mussa alipohudhuria Katika Sherehe za Mahafali ya 3 ya Chuo cha Mafaunzo ya Amali Daya Mtambwe Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Alisema Mafunzo ya Amali ni muhimu sana katika kumtayarisha kijana kwa kazi ili aweze kumudu ushindani katika soko la Ajira kwenye sekta za umma, binafsi na hata kujiajiri mwenyewe.

“Ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana ni moja kati ya changamoto ya Taifa letu. Kwa kulijua hilo, ndio maana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikaazisha Vyuo hivi vya Amali ili vijana wajipatie Taaluma za Ufundi na Stadi za maisha ili waweze kujiajiri katika mazingira yao”alisema Lela.


Aliongeza kuwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imejiwekea malengo mahususi ya kuhakikisha kwamba mfumo wa Elimu inayotolewa katika taasisi zote za Elimu za Zanzibar kuanzia ngazi ya chini hadi Elimu ya juu unalenga kwenye misingi ya Elimu bora.

Aidha alisema Mafunzo haya huisaidia jamii katika kuleta Maendeleo na kuepuka vitendo viovu kama vile, wizi uasharati, ujambazi, utumiaji wa madawa ya kulevya na vitendo vingine viovu ambavyo huhatarisha amani na usalama wa nchi na kudumaza maendeleo.

Alitawataka wahitimu hao kuwa na heshima na nidhamu katika kazi zao ikiwemo kuwahishimu wateja na waajiri wako.

Aliwaasa wazazi kuwekeza katika kuwapatia mafunzo ya Amali katika vyuo vya Serikali ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuweza kuwasaidia wazazi na familia zao.

Alitoa wito kwa jamiii na wahitimu kuedelea kuilinda amani iliyopo katika kipindi hichi na kipindi kijacho cha uchaguzi ili jamii iweze kubaki salama.

Aliwataka wahitimu hao kujikusanya kwa vikundi ili waweze kupatiwa mkopo usio na riba ili kuendeleza mafunzo waliyopewa sambamba na kujiajiri.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka ya Mafunzo ya Amali Zanzibar Dkt. Bakari Ali Silima Amesema Mamlaka ya Mafunzo ya Amali imekuwa inshirikiana na wadau mbali mbali wa ndani na nje ya nchi katika kuimarisha mafunzo ya Amali na kuwapatia ujuzi na fursa zaidi za ajira vijana wetu.

“Mamlaka tayari imesha anza mradi na ENABEL. Mradi huu unatoa mafunzo ya muda mfupi kwa vijana juu ya kilimo cha mwani na kuusarifu, kusindika na kusarifu dagaa, Kufanya matumizi mbadala (recycling) ya mabaki ya vyuma na mbao yanayozalishwa katika karakana zetu na za jamii kwa lengo zima kuhifadhi mazingira” alisema
Alitaja Jumla ya vijana 320, wenye umri wa miaka 18-35, wa Wilaya zote nne za Pemba watanufaika na mradi huu. Pia mradi huu utakuwa na kipengele cha kuendeleza Walimu na kuweka vifaa vya karakana.

“Mamlaka ya Mafunzo ya Amali ipo tayari kushirikiana na Wadau wengine mbali mbali, kwa hali na mali katika kuimarisha mafunzo ya amali ili Chuo kiweze kupiga hatua zaidi”.


Vile vile alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeweka utaratibu mzuri wa kuwapatia mikopo isiyo na riba kwa wote wanaohitaji baada ya kuandika miradi yao ya kujiajiri. Ambapo Hadi sasa kuna vikundi 28 vya wahitimu wa mafunzo ya Amali.

Naye Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Daya Ndugu Saada Ali Hamad, Amesema Kwa sasa Chuo cha Mafunzo ya Amali cha Daya, kinatoa Mafunzo ya Amali ya fani 10, ampapo Katika mwaka 2023 Chuo hiki kilikuwa kinatoa ujuzi katika fani sita tu, ambazo ni: Electroniki, Kilimo, Uvuvi, Useremala, front office operation, na Ufundi wa Magari. Kwa Kuanzia mwaka 2024 tuliongeza fani nyengine 4 za Ufundi wa Umeme wa Magari, Ushoni, TEHAMA na Upishi.
“Kuongezwa kwa fani hizi mpya kwa Chuo cha Daya, na vyuo vyengine kwa ujumla wake, ni Juhudi za makusudi za kuvitanua ya soko la ajira katika jamii. vyuo vya Mafunzo ya Amali vilivyopo ili viendane na mahitaji halisi”.

Moja kati ya mafanikio Makubwa Yaliopatikana ni kuwapatia kwa vitendo Mafunzo ya Amali ambapo jumla ya vijana 521 wamepatiwa mafunzo ya ujuzi na 473 wakiendelea na mafunzo yao chuoni.


Nae, Mratibu wa Mafunzo ya Amali Pemba Ndugu Othaman Zaid Othman Alisema Mafanikio Makubwa yaliopatikana ni uwepo kwa vifaa vya Masomo jambo lilopelekea wahitimu hao kufaulu vizuri hasahasa katika mafunzo ya Vitendo.

Akisoma Risala ya Wahitimu, Mwanafunzi Bayana Kidunhu alielezea changamoto zao ni pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara ya kivumoni , ukosefu wa msikiti katika eneo la chuo na ukosefu wa kituo cha afya katika eneo la chuo.

Alisema wanaishukuru Serikali ya Mapnduzi ya Zanzibar kwa kuwaekea vyuo hivyo ambavyo vimekua ni Mkombozi wao wa maisha kupitia ujuzi walioupata.


Jumla vijana wapatao 136, W’ke 61 sawa na 45% na W’me 75, ambao wanahitimu mafunzo yao katika fani mbali mbali zikiwemo fani za; Useremala, ufundi wa magari, Ufundi elektroniki, Uvuvi, Kilimo, Upishi pamoja na Ukarimu.

Mapema Mhe. Lela amepata fursa ya kutembelea Mabanda ya Maonesho ya kazi za Vitendo zilizoandaliwa na wanafunzi hao pamoja na kupokea Maandamano ya wahitimu hao.

Pia Mhe Lela, Alipata Fursa ya kuwakabidhi Hundi Vikundi viwili vya Ushirika Kwa Upande Pemba.

Hundi hizo zenye Thamani ya Shilingi 14,073,000 zimekabidhiwa kwa wanavikundi viwili vya
Blue Marine Cooperative, kupitia Mradi wa Uuzaji wa vipuri vya mashine za boti ambapo wamekabidhiwa
Kiasi cha mkopo wa Shilingi 8,073,000, Wahitimu wa Chuo cha Amali Daya Na na Kwa Upande wa Kikundi cha Pili ni Ranzi Traders Electrical Rapair Cooperative chenye
Mradi wa kutengeneza vifaa vya umeme Kiasi cha mkopo 6,000,000, Wahitimu wa chuo cha Amali Vitongoji.

Fedha hizo zilizotolewa na Mamlaka ya Mafunzo ya Amali ikiwa ni Moja ya Mikakati yake ya Kuwapatia Mikopo Vikundi vya Ushirika vya Wahitimu, kwa Lengo la kuendeleza Biashara na Kukuza fani walizosomea.

Scroll to Top