The Revolutionary Government of Zanzibar
VOCATIONAL TRAINING AUTHORITY

Mahafali ya Pili(2) Chuo cha Mafunzo ya Amali Makunduchi.

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC) Ndugu Soud Said Ali Amesema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wakala wa Uwezeshaji Wanachi Kiuchumi ZEEA Ipo tayari kuwapatia Mikopo wahitimu wa Mafunzo ya Amali ambao wameunda vikundi vya kujiajiri katika kutekeleza taaaluma zao.

Aliyasema hayo wakati akizungumza mbele ya wahitimu hao katika Mahafali ya pili (2)ya chuo cha Mafunzo ya Amali Makunduchi huko Mkoa wa kusini Unguja.

Aliwataka wahitimu hao kutumia mikopo hiyo kwa malengo waliyopatiwa na kutumia vizuri fedha hizo ili wafanye marejesho kwa uzuri ili wanzao na wao wapate mikopo hiyo.

Aliwaasa wanafunzi na wahitimu kudumisha amani iliyopo nchini na wasikubali kutumika vibaya huko mitaani wanakokwenda, kwani amani ndio msingi wa maendeleo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Dkt. Bakari Ali Silima Amesema, Mafunzo ya Amali hutolewa kutokana na soko la ajiari kwani mamlaka inawwezesha vijana kupitia ujuzi wanaopatiwa kuweza kujiaji na kuajirika.

Alisema Mamlaka ina fanya kazi kubwa kuwahamiasiha jamii juu kujiunga na vyuo hivyo kwani kupitia vyuo hivyo vina nafasi kubwa ya kujifunza kivitendo kupitia karakana za kijfunzia zilizopo vyuoni humo.

Aidha alisema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ipo pamoja na wahitimu hao kwa kuwawezesha na kuwapa mikopo isiyo na riba kwa lengo la kujiendeleza katika kuleta maendeleo.

Hivyo alichukua fursa hii kuwataka wahitimu hao kuuunda vikundi na kuwasilisha miradi ya kujiajiri ili waweze kujipatia mikopo hiyo, kwani kwa sasa jumla ya vikundi 32 tayari vimeshapatiwa mikopo hiyo.

Mkurugenzi vyuo na Mafunzo kutoka Mamlaka ya Mafunzo ya Amali Mhandisi Abdalla Mohammed Hambali, amesema vijana wanaojitimu wamekamlika kwa kuweza kuwa na weledi katika fani zao.

Aliwataka wanafunzi hao kutumia mafunzo hayo vizuri pamoja na kuzingatia maadili katika utendaji kazi wao.

Akisoma Risala ya wafanyakazi Mwalimu Khadija Seleiman Shauri, alisema chuo hicho kimeendelea kupata mafanikio kutokana na kuwaandaa vijana hao waweze kujiajiri na kuajiriwa baada ya kuhitimu mafunzo yao
Alisema chuo kinatoa fani mbali mbali ikiwemo umeme, agro mekaniki, Upishi,Uhunzi, uvuvi na Kilimo, mafunzo yote hayo hutolewa kwa asilimia 70 ni kwa vitendo zaidi.

Akitaja changamoto zinazowakabili kwa sasa ni uhaba ni komputer ambao unapunguza ufanisi wa kufanikisha mafunzo hayo.

Chuo cha Mafunzo ya Amali kimeanzishwa 2022 ambapo kwa mwaka huu jumla wa wanafunzi 98 wanawake 30 na 68 wamehitimu masomo yao katika fani mbali mbali na kukabidhiwa vyeti vyao.

Mamlaka ya Amali inasimamia jumla ya vyuo vitano Unguja na Pemba ambapo kwa mwaka huu Jumla wahitimu 702 wamehitimu kwa mwaka huu.

Scroll to Top